Amnesty Internationa: Idadi ya watu wanaonyongwa duniani inaongezeka
https://parstoday.ir/sw/news/world-i112374-amnesty_internationa_idadi_ya_watu_wanaonyongwa_duniani_inaongezeka
Shirika la Msamaha Duniani (Amnesty International) limetangaza kuwa, idadi ya watu wanaokabiliwa na adhabu ya kifo na kisha kunyongwa imeongezeka duniani.
(last modified 2024-05-30T23:01:21+00:00 )
May 30, 2024 23:01 UTC
  • Amnesty Internationa: Idadi ya watu wanaonyongwa duniani inaongezeka

Shirika la Msamaha Duniani (Amnesty International) limetangaza kuwa, idadi ya watu wanaokabiliwa na adhabu ya kifo na kisha kunyongwa imeongezeka duniani.

Shirika hilo la kutetea haki za binadamu lilinakili visa 1,153 vya adhabu ya kunyongwa mwaka 2023, ambalo ni ongezeko la asilimia 31 kutoka 883 mwaka 2022. Ni idadi ya juu zaidi kunakiliwa na Amnesty International tangu 2015, wakati watu 1,634 walinyongwa kote duniani.

Amnesty pia iligundua kuwa hukumu za kifo zilizotolewa ulimwenguni kote ziliongezeka kwa 20% mnamo 2023.

Takwimu zinazotolewa na mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu zinaonyesha kuwa, Saudi Arabia imewanyonga watu 1,100 katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Madola yanayodai kuwa vinara wa haki za binadamu ulimwenguni yamenyamazia kimya ukandamizaji na vitendo vya kunyongwa kiholela wapinzani nchini Saudi Arabia. Nchi nyingine inayotajwa kukandamiza haki za binadamu na kunyonga wanaharakati wa kisiasa na wapinzani ni Bahrain.

Tangu Februari 14, 2011, Bahrain inashuhudia uasi wa wananchi dhidi ya utawala wa kifalme wa Al-Khalifa. Wananchi wa Bahrain wanataka uhuru, upatikanaji haki na uadilifu, kuondolewa ubaguzi na kuingia madarakani mfumo wa utawala waliouchagua kwa kura zao. Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameshalaani mara kadhaa hatua ya serikali ya Bahrain ya kuwakandamiza wapinzani na kutaka yafanyike mageuzi katika mfumo wa kisiasa wa nchi hiyo.