OCHA: Misaada ya kibinadamu Gaza haikidhi mahitaji
https://parstoday.ir/sw/news/world-i112448-ocha_misaada_ya_kibinadamu_gaza_haikidhi_mahitaji
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imetangaza kuwa, misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Gaza haitoshi kabisa nae neo hilo linakaribia kutumbikiia katika maafa makubwa ya kibinadamu.
(last modified 2024-06-01T22:57:12+00:00 )
Jun 01, 2024 22:57 UTC
  • OCHA: Misaada ya kibinadamu Gaza haikidhi mahitaji

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imetangaza kuwa, misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Gaza haitoshi kabisa nae neo hilo linakaribia kutumbikiia katika maafa makubwa ya kibinadamu.

Taarifa ya OCHA imeeleza kuwa, wakati jeshi la Israel likiendelea na mashambulizi yake ya anga na mashambulizi ya ardhini huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, wakazi wa maeneo hayo wanapokea misaada kidogo sana kiasi kwamba idadi ya watoto wanaokufa kwa njaa inaongezeka kila siku.

Tahadhari hiyo imetolewa leo na Jens Laerke, msemaji wa OCHA, katika mkutano wa Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari huko Geneva Uswisi.

Utafiti wa hivi karibuni wa Umoja wa Mataifa umeonyesha kuwa asilimia 95 ya watoto wenye umri wa miezi sita hadi 23 yaani, hasa wale walio chini ya umri wa miaka mitano hula milo miwili au chini ya hapo kwa siku jambo ambalo ni hatari mno kwa afya zao.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA imeendelea kusisitiza kuwa wajibu wa mamlaka ya Israel ni kuandaa mazingira ya upelekaji misaada bila ya vizingiti.

Mnamo Mei 7, jeshi la utawala wa Kizayuni lilifanya uvamizi na shambulio la nchi kavu dhidi ya mji wa Rafah ulioko kusini mwa Ukanda wa Gaza na kukifunga kivuko cha mji huo cha baina ya Gaza na Misri, ambacho kinachukuliwa kuwa moja ya njia muhimu zaidi za kupitishia misaada ya kibinadamu kuelekea eneo hilo la Palestina.