Aug 03, 2024 04:28 UTC
  • Afisa wa zamani wa CIA: Mauaji ya Haniyeh yamefanyika kwa msaada wa Marekani na Uingereza

Larry C. Johnson, afisa mstaafu wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), amesema kuwa mauaji yalioyofanywa na Israel dhidi ya Ismail Haniyeh, mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas, yamevuka mstari mwekundu na kuongeza kuwa mauaji hayo yametekelezwa kwa taarifa na msaada wa Uingereza na Marekani.

Larry Johnson ameongeza kuwa: "Mvutano wa sasa katika eneo la Magharibi mwa Asia ni mkubwa zaidi ya kile kilichotokea baada ya shambulio la Israel mwezi Aprili kwenye ubalozi mdogo wa Iran huko Damascus."

Katika muktadha huo huo, afisa huyo wa zamani wa CIA amesema: Katika kukabiliana na shambulio la mwezi Aprili, Iran ilituma ujumbe wa wazi kabisa kwa Israel kwamba katika siku zijazo, hatua zozote za kichokozi na za kuzusha mizozo zitakabiliwa na jibu kali.

Johnson ameongeza kuwa: "Hizbullah na Iran zimechokozwa na Israel, kwa upande mwingine, Tel Aviv inapiga mahesabu ya nguvu ya Muqawama mbele ya shambulizi lolote tarajiwa."

Afisa huyo wa zamani wa CIA amesisitiza kuwa, hali ya sasa ni hatari sana.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran tayari imemfahamisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, kwamba itauadhibu utawala wa Kizayuni wa Israel katika fremu ya haki yake ya kujilinda dhidi ya mchokozi. 

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Ali Bagheri Kani amemwambia katibu Mkuu wa UN kwamba: "Kitendo cha kigaidi cha utawala wa Kizayuni cha kumuua Ismail Haniyeh mjini Tehran kimekiuka mamlaka ya kitaifa ya Jamhuri ya Kiislamu na kuhatarisha amani na usalama wa kieneo na kimataifa."

Ali Bagheri Kani

Amesisitiza kuwa: "Iran haitaacha haki yake ya asili ya kujilinda na kuchukua hatua za kujibu za kuwaadhibu Wazayuni wahalifu."

Tags