Maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina yafanyika Berlin Ujerumani
(last modified Mon, 09 Sep 2024 02:54:27 GMT )
Sep 09, 2024 02:54 UTC
  • Maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina yafanyika Berlin Ujerumani

Maelfu ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Ujerumani, Berlin, na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina hususan wa Ukanda wa Gaza.

Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu sambamba na kulaani jinaii za Israel wametangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina.

Vilevile waandamanaji hao wakiwa na bendera ya Palestina wamesisitiza juu ya udharura wa kusitishwa mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza na kukombolewa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na wazayuni maghasibu.

Maandamano mengine makubwa kama hayo yameshuhudiwa nchini Uingereza na Uholanzi ambapo waandamanaji wamepaza sauti za kulaani mauaji ya kimabari ya Israel dhidi ya wananchi wa Palestina.

Waandamanaji hao wametoa mwito pia wa kuchukuliwa hatua za haraka kukomeshwa jinai hizo zilizo dhidi ya binadamu na kuhakikisha kuwa, waliohusika na mauaji hayo wanafikiwa na mkono wa sheria.

 

Mauaji hayo ya kimbari ya utawala wa Kizayuni yanakaribia kutimiza mwaka mmoja tangu tarehe 7 Oktoba, mwaka uliopita wakati utawala huo katili wa Israel ulipoanzisha mashambulizi ya kila upande katika ukanda huo ambapo umedondosha

Kiitengo cha lishe katika Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) kimesema kuwa zaidi ya watoto elfu 50 katika Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na utapiamlo mkali na wanahitaji matibabu ya haraka.