Ireland kuwa na balozi wa kwanza wa Palestina
(last modified Thu, 07 Nov 2024 02:28:51 GMT )
Nov 07, 2024 02:28 UTC
  • Ireland kuwa na balozi wa kwanza wa Palestina

Serikali ya Ireland imeafiki kuteuliwa balozi wa Palestina kwa mara ya kwanza katika nchi hiyo ya bara Ulaya.

Duru za karibu na serikalii ya Ireland zimethibitisha kwamba Jilan Wahba Abdul-Majid ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Ujumbe wa Palestina nchini Ireland anakuwa balozi wa Palestina nchini humo.

Hivi karibuni, Ireland ikiwa pamoja na Norway na Uhispania zilitangaza kulitambua rasmi taifa la Palestina, jambo ambalo liliukasirisha sana utawala haramu wa Israel. Ireland ni miongoni mwa nchi chache za Ulaya ambayo imekuwa mstari wa mbele kuwaunga mkono wa Palestina.

Majuzi Rais Michael D. Higgins wa nchi hiyo, alilaani vikali kitendo cha walowezi wa Kizayuni cha kuishambulia misafara ya misaada ya kibinadamu inayopelekwa Ukanda wa Gaza na kusema kuwa mashambulizi hayo yanafanyika wakati Wapalestina wa Gaza wanateseka kwa njaa.

Aidha Ireland imekuwa ikishuhudia maandamano ya mara kwa mara ya waungaji mkono wa Palestina wanaoandamana na kupiga nara kulaani jinai na mauajii ya kimbari ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.