Jordan avunja kimya, akemea mauaji ya Wamarekani weusi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i12043-jordan_avunja_kimya_akemea_mauaji_ya_wamarekani_weusi
Nyota wa zamani wa mchezo wa mpira wa kikapu nchini Marekani, Michael Jordan amevunja kimya chake kuhusu mauaji yanayofanywa na polisi wazungu wa nchi hiyo dhidi ya Wamarekani weusi na taathira mbaya za mauaji hayo ya kibaguzi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 26, 2016 12:26 UTC
  • Jordan avunja kimya, akemea mauaji ya Wamarekani weusi

Nyota wa zamani wa mchezo wa mpira wa kikapu nchini Marekani, Michael Jordan amevunja kimya chake kuhusu mauaji yanayofanywa na polisi wazungu wa nchi hiyo dhidi ya Wamarekani weusi na taathira mbaya za mauaji hayo ya kibaguzi.

Michael Jordan amesema katika barua iliyochapishwa na mtandao wa The Undefeated unaosimamiwa na kanali ya televisheni ya ESPN  kwamba anajua Marekani inaweza kuwa boza zaidi kuliko hivi sasa na kwamba hawezi tena kunyamazia kimya mauaji yanayofanywa na polisi dhidi ya watu wenye asili ya Afrika. Jordan amesema yeye kama Mmarekani aliyepoteza baba yake katika matukio ya kikatili na utumiaji mabavu na kama mtu mweusi, anasikitishwa sana na mauaji yanayofanywa na polisi dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika na kuhuzunishwa na harakati za chuki zinazowaua polisi.

Polisi Marekni wakimfyatulia risasi raia

Nyota huyo wa zamani wa mpira wa kikapu wa Marekani katika muongo wa 1980 na 90 ametoa msaada wa dola milioni mbili kwa taasisi mbili za Uhusiano wa Polisi na Jamii na Mfuko wa Kulinda Haki wa NAACP na kusema: Japokuwa msaada huo hautoshi kutatua matatizo hayo lakini anatarajia kuwa, fedha hizo zitazisaidia jumuiya hizo mbili kukomesha hitilafu zilizopo.

Shakhsia na jumuiya mbalimbali nchini Marekani na nje ya nchi hiyo zimekuwa zikilalamikia mauaji yanayowalenga Wamarekani wenye asili ya Afrika. Mauaji hayo yanayotajwa kuwa ni ya kibaguzi yanafanywa na polisi wazungu.