Msaidizi wa Papa Francis atuhumiwa kuwalawiti watoto
(last modified Fri, 29 Jul 2016 04:17:57 GMT )
Jul 29, 2016 04:17 UTC
  • Msaidizi wa Papa Francis atuhumiwa kuwalawiti watoto

Polisi nchini Australia inachunguza madai ya liwati dhidi ya Mkuu wa Hazina ya Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Duniani Vatican, Kadinali George Pell.

Kwa mujibu wa shirika la habari la taifa la Australia ABC, polisi katika jimbo la Victoria wameanzisha uchunguzi dhidi ya Kadinali Pell ambaye anasemekana kuwa mpambe wa karibu wa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis, wa tuhuma za kuwalawiti vijana wadogo wa kiume katika shule moja ya msingi mjini Ballarat eneo la Torquay alipokuwa padri katika kanisa moja la Kikatoliki la eneo hilo. Tayari familia, walalamikaji na walioshuhudia vitendo hivyo vya unyanyasaji wamerekodi taarifa katika kituo cha polisi jimboni Victoria.

Hata hivyo Kadinali Pell mwenye umri wa miaka 75 amekanusha tuhuma dhidi yake na kusema kuwa katika maisha yake hawajahi kumdhulumu yeyote kimapenzi, kunajisi au kulawiti.

Viongozi wa Kanisa Katoliki wamekuwa wakituhumiwa kuwalawiti watoto wadogo

Hii ni katika hali ambayo, miezi michache iliyopita, Dayosisi Kuu ya Kanisa Katoliki katika mji wa Baltimore jimboni Maryland nchini Marekani ilifichua majina ya makasisi 71 wanaotuhumiwa kuwalawiti watoto wadogo.

Papa Francis, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani

 

Kwa mujibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Marekani, takriban makasisi 6,900 wa Kanisa Katoliki la Roma wanadaiwa kuwalawiti watoto wadogo 16,900 kati ya mwaka 1950 na 2011.

Tags