Waandamanaji wachoma moto nyumba ya mwasisi wa Bangladesh, Sheikh Mujibur Rahman
Kundi kubwa la waandamanaji jana liliharibu na kuchoma makazi ya mwasisi wa Bangladesh, Sheikh Mujibur Rahman huko Dhaka, wakati binti yake, Sheikh Hasina waziri mkuu aliyeondolewa madarakani alipokuwa akihutubia kwa njia ya mtandao.
Nyumba ya Sheikh Mujibur Rahman ilichomwa moto wakati binti yake Hasina alipokuwa akitoa hotuba ambayo iliandaliwa na Jumuiya ya Awami ya wanafunzi iliyovunjwa na sasa inajulikana kama Chhatra League, akiwataka wananchi kuanzisha harakati ya upinzani dhidi ya serikali ya sasa ya Bangladesh inayoongozwa na Muhammad Yunus, mshindi wa Tuzo ya Nobel.
Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Bangladesh aliyeuzuliwa madarakani ameongeza kuwa: Waandamanaji wanaweza kubomoa nyumba lakini si historia; na wanapasa kukumbuka kuwa historia inalipiza kisasi.
Vuguvugu la wanafunzi hapo awali liliahidi kufuta Katiba ya Bangladesh ya mwaka 1972 na kuizika "katiba ya Mujib" huku baadhi ya makundi yenye siasa kali ya mrengo wa kulia yakipendekeza kubadilishwa wimbo wa taifa uliopitishwa na serikali iliyoongozwa na Sheikh Mujib baada ya uhuru.
Sheikh Hasina amesema kuwa waandamanaji hao bado hawajapata nguvu ya kuharibu bendera ya taifa, katiba na uhuru wao ambapo mamilioni ya wananchi wa Bangladesh walisabilia maisha yao kwa ajili ya kuikomboa nchi yao.
Nyumba hiyo ni alama mashuhuri ya muda mrefu katika historia ya Bangladesh, kwani Sheikh Mujibur Rahman aliongoza harakati za uhuru kwa miongo kadhaa kutoka katika nyumba hiyo wakati wa utawala wa Jumuiya ya Awami, ilipogeuzwa kuwa jumba la makumbusho na kutembelewa mara kwa mara na wakuu wa nchi za kigeni au watu mashuhuri, kulingana na itifaki ya serikali.