Vita vya ushuru vya Trump: Scholz aapa kujibu mapiga papo hapo
(last modified Tue, 11 Feb 2025 02:44:36 GMT )
Feb 11, 2025 02:44 UTC
  • Vita vya ushuru vya Trump: Scholz aapa kujibu mapiga papo hapo

Kansela wa Ujerumani ameonya kwamba iwapo Marekani itaweka ushuru wa ziada kwa bidhaa za Umoja wa Ulaya (EU), watu wa Ulaya watajibu mapigo "ndani ya saa moja."

Olaf Scholz ameyasema hayo katika mdahalo wa uchaguzi na Friedrich Merz, kiongozi wa chama cha kihafidhina cha Christian Democratic Union, akijibu maswali ya waandishi habari kuhusu uwezekano wa Trump kuzidisha ushuru wa forodha dhidi ya nchi za Ulaya. 

Kansela wa Uujerumani aliongeza kuwa: "Sisi katika Umoja wa Ulaya tutachukua hatua ndani ya saa moja."

Rais wa Marekani, Donald Trump amekuwa akiwatishia washirika wa nchi hiyo kuwawekea ushuru ziada wa bidhaa zao zinazoingizwa nchini Marekani. Wiki iliyopita, alitangaza ushuru wa ziada dhidi ya China, Mexico na Canada, lakini saa kadhaa baadaye alitangaza kusimamishwa kwa mwezi mmoja ushuru ziada kwa Mexico na Uchina baada ya nchi hizo kujibu mapigo.

Pia ametishia kuiwekea Ulaya ushuru zaidi. Kufuatia vitisho vya Trump, viongozi wa Umoja wa Ulaya walifanya mkutano mjini Brussels, nakujadiili tishio la ushuru la Marekani.

Tume ya Ulaya pia ilikuwa imemuonya Trump kwamba "Umoja wa Ulaya utatoa jibu kali kwa mshirika yeyote wa kibiashara ambaye anaweka ushuru usio wa haki au wa kiholela kwa bidhaa za jumuiya hiyo."