UN yatuma salamu za pole na rambirambi kwa wananchi na serikali ya Iran kufuatia mripuko wa Bandar Abbas
(last modified Sun, 27 Apr 2025 07:43:46 GMT )
Apr 27, 2025 07:43 UTC
  • UN yatuma salamu za pole na rambirambi kwa wananchi na serikali ya Iran kufuatia mripuko wa Bandar Abbas

Umoja wa Mataifa umetuma salamu za pole kwa wananchi na serikali ya Iran kufuatia mripuko mkubwa uliotokea katika bandari ya Shahidi Rajaee kusini mwa Iran jana Jumamosi.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema kuhusu mripuko uliotokea katika Bandari ya Shahid Rajaee huko Bandar Abbas, Iran: "Tumesikitishwa sana watu wengi walioathirika katika mripuko wa jana uliotokea katika Bandari ya Shahid Rajaee huko Bandar Abbas katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran".

Dujarric amesema: Tunatoa pole  kwa familia za wahanga, wananchi na serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na tunawatakia afueni ya haraka majeruhi wote. 

Mripuko mkubwa uliotokea jana katika bandari ya Shahidi Rajaee huko Bandar Abbas hadi sasa umesababisha vifo vya watu 25 na majeruhi zaidi ya 800. Kwa mujibu wa Press TV, mripuko huo ulitokea baada ya lori la mafuta kulipuka katika bandari ya Shahid Rajaee katika Mkoa wa Hormozgan kwa sababu ambazo hazijajulikana hadi sasa.  

Kwa mujibu wa ripoti za awali, timu za uokoaji na huduma za kwanza zilifika kaika eneo la tukio na oparesheni za uchunguzi na usaidizi zingali zinaendelea.