Ripoti: Mfumo wa elimu wa Uingereza unahitaji kukombolewa kutoka kwenye ukoloni
(last modified Mon, 28 Apr 2025 02:24:07 GMT )
Apr 28, 2025 02:24 UTC
  • Ripoti: Mfumo wa elimu wa Uingereza unahitaji kukombolewa kutoka kwenye ukoloni

Mauaji ya kimbari yanayofanywa dhidi ya Wapalestina katika kipindi cha miezi 18 sasa yasingewezekana bila ya kuwadhalilisha watu wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwa kuwatambua kuwa sio binadamu katika vyombo vya habari na miongoni mwa wanasiasa hasa wa nchi za Magharibi wanaoungwa mkono na Harakati ya Kimataifa ya Kizayuni.

Haya yamasemwa na wataalamu walioandaa mkutano wa Chelmsford wanaosisitiza udharura wa kukombolewa mfumo wa elimu wa Uingereza na nchi nyingine za Magharibi kutoka kwenye mfumo wa ukoloni.

Kwa mujibu wa tafsiri yao ya ada na desturi za Kiyahudi, Wapalestina wanahesabiwa kuwa ni goyim, (watu wasio Wayahudi) na wa mataifa mengine, na hivyo wanatambuliwa kuwa sio binadamu, suala ambalo linafanya mauaji ya umati dhidi ya Wapalestina yakubalike kwa wale wanaohusika.

Msingi wa kudhalilisha utu wa Wapalestina na kuwatambua kuwa sio binadamu ni mfumo wa elimu ambao unafadhilisha na kuona roho za baadhi ya watu kuwa ni bora na juu ya nyingine, na hilo ndilo jambo ambalo waandaaji wa mkutano wa Chelmsford, Uingereza wanataka kulibadilisha.

Wanasema wanalenga kufanya kazi ya kuondoa ukoloni katika mfumo wa elimu wa Uingereza wenye ubaguzi wa rangi ambao unaathiriwa pakubwa na harakati ya Kizayuni.

Wanafunzi Uingereza

"Ili kuua watu wengi zaidi, inabidi uwawasilishe kama sio binadamu haswa, kama Amaleki, kama alivyotamka Benjamin Netanyahu", amesema msomi David Miller na kuongeza: "Kwa hakika hilo linatokea Israel kama tunavyojua sisi sote, lakini pia linatokea nchini Uingereza na katika nchi nyingine pia, ambako Wazayuni wanatumia muda mwingi na juhudi kubwa kujaribu kutuaminisha kwamba Wapalestina si binadamu kamili, kwamba Waislamu si binadamu kamili, na huo ni mchakato unaoendelea mashuleni."

Wanajopo wa mkutano wa Chelmsford, Uingereza wanasema ni muhimu kuunga mkono walimu, sio tu kushughulikia masuala ya ukoloni na ubaguzi wa rangi kwa undani zaidi, lakini pia kupinga mashinikizo kutoka kwa wakuu wao linapokuja suala la kushughulikia masuala kama Uzayuni.