Pezeshkian: Iran iko tayari kupanua mahusiano na Afrika katika nyanja zote
Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amezungumzia uwezo wa bara la Afrika na ulazima wa kuwepo ushirikiano na kwamba, Iran iko tayari kupanua ushirikiano wake na bara la Afrika katika nyanja zote.
Daktari Pezeshkian amesema hayo katika Mkutano wa 3 wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Iran na Afrika na kueleza kuwa Iran iko tayari kuzishirikisha nchi za Afrika mafanikio yake katika nyanja mbalimbali.
Rais Pezeshkian ameongeza: "Watu wote wanapaswa kusaidiana, kuunganisha mikono, na kujenga nyumba iliyojaa amani, upendo, huruma, uhuru na ubinadamu na kwamba, badala ya kupanda mbegu za chuki na uadui, wanapaswa kuunda urafiki, upendo, imani, urafiki na udugu."
Rais wa Iran amesisitiza kuwa: "Kwa bahati mbaya, kuna kundi la wavamizi na wachochezi ambao wanakiuka haki za wengine na kufanya jinai. Walilifukuza na kuua kundi kutoka katika ardhi yao na kutilia alama ya swali ubinadamu." Nyuma ya nyuso zao za kibinadamu, hawa ni viumbe wakatili na wauaji zaidi duniani, na wanawaua watu wasio na hatia, wanawake na watoto, wazee kwa vijana, bila hofu yoyote.

Mkutano wa 3 wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Iran na Afrika umeanza leo hapa Tehran na utaendelea hadi tarehe 29 mwezi huu wa Aprili. Mkutano huu aidha utaendelea katika mji wa Isfahan hapa nchini tarehe 29 hadi 30 Aprili.
Mkutano wa 3 wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Iran na Afrika unaangazia maeneo makuu manne: Mafuta- gesi- petrokemikali, sekta ya madini, kilimo na nishati.
Mkutano wa tatu wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Iran na Afrika unafanyika kwa wakati mmoja na Maonyesho ya Iran ya Expo 2025. Mkutano huu umetajwa kuwa fursa kwa wageni kutoka Afrika ili kufahamu uwezo na suhula za Iran ikiwa ni pamoja na bidhaa zinazouzwa na nchi hii katika nchi mbalimbali duniani.