Mataifa masikini yakabiliwa na wimbi la madeni ya China
Mataifa masikini duniani sasa yanakabiliwa na wimbi kuubwa la madeni ya China na kuyaweka katika hali mbaya kutokana na kulemewa na madeni hayo.
Ripoti iliyochapishwa na shirika la kimataifa nchini Australia imetaja hali ngumu ya kiuchumi inayoyakabili mataifa masikini duniani kutokana na mzigo wa madeni ya China, ambayo mwaka huu wa 2025 yamevunja rekodi.
Taasisi ya Lowly inayofuatilia kiwango cha madeni ulimwenguni imesema katika ripoti yake kwamba, mradi wa miundombinu wa China, maarufu kama BRI, uliotoa mikopo mikubwa kwa ajli ya ujezi wa bandari, reli, barabara na majengo katika mataifa ya Afrika, Asia na Pasifiki, umesababisha kiwango kikubwa cha madeni kwa mataifa hayo yanayoendelea.
Mzigo huo wa madeni umekuwa na taathira mbaya kwa Uchumi wa baadhi ya mataifa hayo ambayo sasa yanalazimika kujikita katika kulipa madeni hayo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ndani ya muongo huu, China itakuwa mnufaika mkubwa zaidi wa kukusanya madeni yake badala ya kuwa muwekezaji kwenye mataifa hayo, huku nchi zilizokopeshwa zikiingia kwenye wimbi kubwa la ufukara kutokana na kulipa madeni hayo.