Marekani yatumia kura ya veto kupinga azimio la kusitisha vita Gaza
Marekani imetumia kura turufu kuzuia kupasishwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka usitishwaji vita Gaza, kuwezesha ufikaji wa misaada ya kibinadamu na kuachiliwa kwa mateka.
Azimio hilo ambalo rasimu yake ilianza kujadiliwa tangu mwezi uliopita wa Agosti, liliungwa mkono na wanachama wote 14 wa baraza hilo ispokuwa Marekani licha ya ripoti zote kuonyesha kuwa, hali ya kibinadamuu katika Ukanda wa Gaza ni mbaya mno.
Hii ni kura ya turufu ya sita ya Marekani tangu Israel ilipoanzisha hujuma ya kinyama dhidi ya ukanda wa Gaza.
Mwezi Juni, Marekani ilitumia pia kura yake ya turufu kuzuia azimio kama hilo ili kumlinda mshirika wake Israel. Mwanadiplomasia wa Marekani Morgan Ortagus ametetea uamuzi wa taifa lake akidai kwamba azimio hilo halikujumuisha kauli za kulaani vitendo vya Hamas na kuwa limeshindwa kutambua hali halisi na ukweli kwamba, eti kumekuwa na ongezeko kubwa la mtiririko wa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.
Hii ni katika hali ambayo, ripoti zote za masharika ya misaada yua kibinadamu zinaonyesha kuwa, utawala wa kizayuni wa Israel umekwamishha pakubwa zoezi la upelekaji wa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza na hata imekuwa ikitumia njaa kama silaha ya kuwaua Wapalestina. Si hayo tu, hata sehemu ndogo ya misaada inayoingia huko Gaza imekuwa mtego wa kifo kutokana na Wapalestina kushambuliwa na kuuawa wakiwa katika safu za kusubiri chakula cha misaada.
Hayo yanajiri wakati Israel imeendeleza operesheni yake kubwa ya kijeshi huko Gaza City huku maelfu ya Wapalestina wakiendelea kuondoka katika jiji hilo na kuelekea eneo la Kusini. Mamlaka za Gaza zimetangaza watu 85 wameuawa shahidi katika kipindi cha saa 24 zilizopita.