Guterres: Ulimwengu haupaswi kutishwa na vitisho vya Israel kuhusu Palestina
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonya kwamba vitisho vya Israel havipaswi kuzuia kutambuliwa rasmni kwa taifa la Palestina.
Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema: Tishio la Israel la kutwaa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan halipaswi kuzuia jamii ya kimataifa kuchukua hatua za kisiasa. Ametahadharisha kuwa uharibifu wa Gaza na upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi unaendelea kuongezeka. Guterres ameitaja hali ya kibinadamu huko Gaza kuwa janga na kusema: 'Hiki ndicho kiwango kibaya zaidi cha vifo na uharibifu ambao nimewahi kuushudia katika kipindi cha uongozi wangu kama Katibu Mkuu. Hata kama baadhi ya mashirika ya Umoja wa Mataifa yamechukulia hatua na jinai za Israel huko katika Ukanda wa Gaza kama mauaji ya halaiki, lakini Guterres amekataa kutumia neno hili na kusema: "Tatizo si neno, bali ni ukweli wa mambo."
Licha ya kuendelea mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya watu wasio na hatia huko Gaza, lakini jamii ya kimataifa na hasa taasisi zilizopewa jukumu la kulinda amani na kuwawajibisha watenda jinai dhidi ya binadamu wakiongozwa na utawala wa Kizayuni, kama Umoja wa Mataifa na hasa Baraza la Usalama, zimeshindwa kabisa kutekeleza jukumu hilo na hivyo kuupa utawala huo wa kigaidi kiburi cha kuendeleza jinai dhidi ya Wapalestina bila kujali lolote.