Ufaransa na nchi nyingine 9 kuitambua rasmi Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/world-i131034-ufaransa_na_nchi_nyingine_9_kuitambua_rasmi_palestina
Katika hatua ya kihistoria, Ufaransa na nchi nyingine tisa zimetangaza kuwa zitalitambua rasmi taifa huru la Palestina.
(last modified 2025-09-20T11:48:43+00:00 )
Sep 20, 2025 11:48 UTC
  • Ufaransa na nchi nyingine 9 kuitambua rasmi Palestina

Katika hatua ya kihistoria, Ufaransa na nchi nyingine tisa zimetangaza kuwa zitalitambua rasmi taifa huru la Palestina.

Serikali ya Paris imetangaza kuwa nchi 10 zitatambua taifa huru la Palestina wiki ijayo. Canada, Australia, Ureno, Ubelgiji, Malta, Luxembourg, San Marino, Andorra na Ufaransa zitashiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Palestina kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York siku ya Jumatatu na kutangaza rasmi uamuzi huo.

Emmanuel Macron pia atatangaza uamuzi wa Ufaransa kuhusu suala hilo siku ya Jumatatu saa 15:00 kwa saa za New York. Huenda Uingereza ikatangaza msimamo wake Jumapili usiku au Jumatatu, na Ureno nayo itatangaza rasmi msimamo wake wa kuitambua Palestina kabla ya mkutano huo. Mshauri wa rais wa Ufaransa ameitaja hatua hiyo kuwa ya kimageuzi katika kutafuta ufumbuzi wa kubuniwa mataifa mawili na kuuita mpango wa Israel wa kunyakua sehemu za Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kuwa "mstari mwekundu" na "ukiukaji wa sheria za kimataifa."