Maelfu waandamana Amsterdam wakihimiza hatua kali dhidi ya Israel
https://parstoday.ir/sw/news/world-i131686-maelfu_waandamana_amsterdam_wakihimiza_hatua_kali_dhidi_ya_israel
Maelfu ya wancnhi wa Uholanzi walikuwa wamevaa mavazi mekundu wameandamana mjini Amsterdam wakiitaka serikali ya Uholanzi kuchukua hatua madhubuti zaidi na kali zaidi dhidi ya Israel na kusaidia kumaliza vita vilivyodumu kwa takriban miaka miwili sasa huko Ghaza, Palestina.
(last modified 2025-10-07T00:56:15+00:00 )
Oct 07, 2025 00:56 UTC
  • Maelfu waandamana Amsterdam wakihimiza hatua kali dhidi ya Israel

Maelfu ya wancnhi wa Uholanzi walikuwa wamevaa mavazi mekundu wameandamana mjini Amsterdam wakiitaka serikali ya Uholanzi kuchukua hatua madhubuti zaidi na kali zaidi dhidi ya Israel na kusaidia kumaliza vita vilivyodumu kwa takriban miaka miwili sasa huko Ghaza, Palestina.

Maandamano hayo, yaliyofanyika chini ya mwezi mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa Uholanzi, yanafuatia mikutano miwili mikuu iliyofanyika mapema mwaka huu huko The Hague ambayo ilivutia makumi kwa maelfu ya watu.

Maandamano ya Amsterdam yameambatana na mwisho wa wiki ya maandamano ya kimataifa, wakati mamia kwa maelfu ya wapenda haki duniani walipoandamana huko Roma, Barcelona na Madrid siku ya Jumamosi, wakilaani mashambulizi ya kijeshi yanayoendelea kufanywa na Israeli huko Ghaza licha ya madai ya kusimamishwa vita.

Maandamano mengine yalifanyika pia katika miji ya Paris, Lisbon, Athens, Skopje, London na Manchester, ikiwa ni kuzidi kuthibitisha kuongezeka hasira na ghadhabu ya kimataifa dhidi ya jinai za utawala wa Kizayuni huko Ghaza.

Siku ya Ijumaa, zaidi ya watu milioni 2 wa Italia walijiunga na mgomo wa umma kulaani jinai na uhalifu wa kuchupa mipaka unaoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina.

Maandamano hayo yamekuja huku Hamas ikisema imekubali kwa masharti mapendekezo ya amani yaliyotolewa na rais wa Marekani Donald Trump.

Hata jana Jumatatu, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ilitangaza katika taarifa yake Jumatatu kuwa timu yake ya mazungumzo imeshawasili Misri ikiongozwa na Khalil al-Hayya, mkuu wa harakati ya Hamas katika Ukanda wa Ghaza, kwa ajili ya mazungumzo kuhusu utaratibu wa usitishaji vita, kuondolewa vikosi vya Israel vinavyoikalia kwa mabavu maeneo ya Ghaza na kubadilishana mateka.