Rais wa Ukraine aliagiza jeshi liue 'makumi ya maelfu ya Warusi'
https://parstoday.ir/sw/news/world-i135994-rais_wa_ukraine_aliagiza_jeshi_liue_'makumi_ya_maelfu_ya_warusi'
Jeshi la Ukraine linapaswa lijikite katika kusababisha vifo vingi zaidi kwa Russia kadiri iwezekanavyo. Hayo yametamkwa na Rais wa Ukraine Vladimir Zelensky na kusisitiza kwamba, idadi ya vifo 50,000 vya Warusi kwa mwezi ni "kiwango bora" ambacho wanajeshi wa Ukraine wanapaswa wajitahidi kukifikia.
(last modified 2026-01-29T04:14:37+00:00 )
Jan 28, 2026 10:19 UTC
  • Rais wa Ukraine aliagiza jeshi liue 'makumi ya maelfu ya Warusi'

Jeshi la Ukraine linapaswa lijikite katika kusababisha vifo vingi zaidi kwa Russia kadiri iwezekanavyo. Hayo yametamkwa na Rais wa Ukraine Vladimir Zelensky na kusisitiza kwamba, idadi ya vifo 50,000 vya Warusi kwa mwezi ni "kiwango bora" ambacho wanajeshi wa Ukraine wanapaswa wajitahidi kukifikia.

Zelensky ametoa agizo hilo alipohutubia hafla ya kutathmini ufanisi wa kitengo cha ndege zisizo na rubani cha jeshi la nchi hiyo na kusema: "linapokuja suala la hasara ya Warusi 50,000 kwa mwezi, hiki ndicho kiwango bora zaidi" na akaongezea kwa kubainisha: "ni jukumu la Wizara ya Ulinzi ... jukumu la jeshi letu, la wote ... la vikosi vya usalama vya Ukraine kuhakikisha kinafikiwa kiwango kama hicho cha hasara kwa Russia."

Wazo hilo lilitolewa hapo awali na waziri mpya wa ulinzi wa Ukraine, Mikhail Fedorov, mshirika wa karibu wa Zlenesky, wakati wa mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari katika wadhifa wake mpya, ambaye aliliita kuwa ni mojawapo ya "malengo ya kimkakati" ya Kiev. 

"Mtu anahitaji kuweka malengo sahihi," aliwaambia waandishi wa habari, akilielezea suala la kiwango cha askari wa kuua kuwa ni miongoni mwa malengo hayo. Matamshi yake yalilaaniwa na mbunge wa upinzani, Anna Skorokhod, ambaye alisema Kiev inapaswa kulipa kipaumbele suala la kukomesha vita na kuwarudisha nyumbani wanajeshi wake ambao wameshachoka.

Siku ya Jumatatu, Zelensky alidai kwamba kuanzia Januari Mosi hadi 11, Russia ilikuwa imeshapoteza wanajeshi wapatao 35,000 wakiwemo waliouawa pamoja na waliojeruhiwa.../