Trump aondoa vitisho baada ya onyo kali kutoka Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i137544-trump_aondoa_vitisho_baada_ya_onyo_kali_kutoka_iran
Rais wa Marekani amelazimika kuondoa vitisho vyake kuhusu kushambulia miundombinu ya umeme ya Iran baada ya onyo kali la Iran.
(last modified 2026-03-24T04:34:11+00:00 )
Mar 24, 2026 04:34 UTC
  • Trump aondoa vitisho baada ya onyo kali kutoka Iran

Rais wa Marekani amelazimika kuondoa vitisho vyake kuhusu kushambulia miundombinu ya umeme ya Iran baada ya onyo kali la Iran.

Baada ya Tump kutoa tishio la kulenga miundombinu ya nishati ya Iran ndani ya saa 48, Iran ilitoa onyo kwamba iwapo vitisho hivyo vingetekelezwa, mashambulizi dhidi ya miundombinu ya umeme na miundombinu muhimu ya utawala wa Kizayuni na ya Marekani katika eneo hili ingelengwa na kuharibiswa kikamilifu na vikosi vya ulinzi vya Iran.

Kufuatia onyo hilo kali kutoka  kuhusu hatua ya kujibu mashambulizi yoyote dhidi ya miundombinu ya nishati au umeme, Trump amelazimika kuondoa vitisho vya kutaka kushambulia vituo vya nishati vya Iran.

Katika ujumbe alioweka kwenye mtandao wake wa kijamii, Trump aliandika kuwa ameagiza kuahirishwa kwa mashambulizi yote yaliyopangwa dhidi ya miundombinu ya nishati ya Iran kwa muda wa siku tano. Aidha, alidai kuwa yuko katika mazungumzo na Iran ili kumaliza vita vinavyoendelea.

Wakati huohuo, chanzo cha Kiirani kilisema kuwa hakukuwa na mawasiliano ya moja kwa moja au yasiyo ya moja kwa moja na Trump, kikiongeza kuwa aliamua kusalimu amri baada ya kufahamishwa kwamba Iran ingesambulia vituo vyote vya umeme katika eneo zima la Asia Magharibi.

Tangu Marekani na Israel zianzishe vita vya kichokozi dhidi ya Iran mnamo Februari 28 sawa na 10 Ramadhani, Iran imekuwa ikipokea ujumbe kutoka wapatanishi kuhusu kusitisha vita ambapo majibu yamekuwa wazi: Iran itaendelea na hatua zake za ulinzi hadi ipate kiwango kinachohitajika cha uwezo wa kuzuia shambulio. Kwa msingi huo, hakuna mazungumzo yaliyofanyika wala yanayoendelea sasa, na kwa mbinu za vita vya kisaikolojia kama hizi, Lango-Bahari la Hormuz halitarudi katika hali yake ya kabla ya vita, wala masoko ya nishati hayatapata utulivu.

Wataalamu wa masuala ya kisiasa wanaamini kuwa shinikizo kutoka masoko ya fedha na sekta ya mafuta na gesi nchini Marekani na katika nchi za Magharibi limeongezeka, na hilo limekuwa miongoni mwa sababu muhimu zilizomsukuma Trump kusalimu amri katika vitisho vyake dhidi ya miundombinu ya umeme ya Iran.