Wakazi wa Roma, Italia waandamana kuonesha mshikamano na Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/world-i138548-wakazi_wa_roma_italia_waandamana_kuonesha_mshikamano_na_palestina
Duru za habari zimeripoti kuwa, idadi kubwa ya raia wanaopiga dhulma na ukandamizaji duniani na waungaji mkono wa mapambano ya ukombozi wa Palestina wameandamana huko Roma mji mkuu wa Italia kulalamikia mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya msafara wa kimataifa kwa jina la The Global Sumud Flotilla kwa lengo la kuvunja mzingiro haramu wa Israel dhidi ya watu wa Gaza.
(last modified 2026-05-22T14:52:33+00:00 )
May 22, 2026 14:50 UTC
  • Wakazi wa Roma, Italia waandamana kuonesha mshikamano na Palestina

Duru za habari zimeripoti kuwa, idadi kubwa ya raia wanaopiga dhulma na ukandamizaji duniani na waungaji mkono wa mapambano ya ukombozi wa Palestina wameandamana huko Roma mji mkuu wa Italia kulalamikia mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya msafara wa kimataifa kwa jina la The Global Sumud Flotilla kwa lengo la kuvunja mzingiro haramu wa Israel dhidi ya watu wa Gaza.

Waandamanaji hao pia wametangaza uungaji mkono wao kwa kadhia ya Palestina.

Kundi hilo la wanaharakati na waandamanaji wa Kitaliano walipiga nara dhidi ya hujuma ya utawala wa Kizayuni ya kushambulia msafara huo wa The Global Sumud Flotilla, wakiituhumu serikali ya Italia kuwa inashirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel. Vilevile wametoa wito wa kusitishwa kikamilifu uhusiano wa kidiplomasia, kibiashara na kijeshi na serikali ya Tel Aviv.

Wanaharakati hao ambao waliandamana katikati ya mji wa Roma wameashiria historia ya miaka 78 ya uvamizi na ukaliaji mabavu wa Israel, mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina, jinai za hivi karibuni dhidi ya watu wa Gaza na shambulio dhidi ya misafara ya misaada katika maji ya kimataifa na kusema: "Hii leo utawala wa Israel si tishio kwa Palestina au Lebanon tu, bali ni hatari kwa binadamu wote na jamii ya kimataifa; na hatua zinapasa kuchukuliwa kukomesha uhalifu wa Israel.

Washiriki katika maandamano ya Roma pia wameitaka serikali ya Italia kukata uhusiano wote wa kibiashara, kidiplomasia na kijeshi na utawala huo unaofanya jinai dhidi ya binadamu.