Simulizi la Wall Street Journal kuhusu vita vya Marekani dhidi ya Iran: Ni ushindi wa kimaonyesho wa Trump au kushindwa halisi?
-
Donald Trump
Mhariri mkuu wa Wall Street Journal amesema: "Trump analazimika kudhihirisha kushindwa kwake mbele ya Iran kama ushindi ili kulinda sura na hadhi yake."
Gerard Baker amesema: Makubaliano tarajiwa na Iran kwa wale wenye msimamo mkali chini Marekani si kitu kingine zaidi ya kusalimu amri. "Ikiwa Trump atakubali mkubaliano ya nyuklia na Iran, atakuwa amesaini mkataba uleule ambao Obama alisaini, baada ya miaka 11 ya ukosoaji wa mara kwa mara dhidi ya mkataba huo. Mkataba uliopo mezani si chochote zaidi ya aibu kubwa kwa Trump," ameandika mhariri wa Wall Street Journal.
Gerard Baker ameongeza kwa kusema: "Trump analazimika kuonyesha kushindwa kwake mbele ya Iran kama ushindi ili kulinda heshima yake; lakini ukweli ni kwamba baada ya mvutano huu wote, Iran bado inadhibiti Mlango-Bahari wa Hormuz."
Wakati huo huo gazeti la New York Times, limeandika katika makala yenye kichwa cha maneno: Is It Over and Done? kwamba Donald Trump anajaribu kuonyesha Vita vya Iran kama vinavyokaribia kuisha na mafanikio kamili. Lakini baada ya miaka mingi ya kujaribu kulazimisha simulizi yake dhidi ya ukweli halisi wa mambo, sasa anakabiliwa na mgogoro ambao hauoani na hadithi yake.