Msikiti wateketezwa moto na wenye chuki dhidi ya Uislamu Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i15232-msikiti_wateketezwa_moto_na_wenye_chuki_dhidi_ya_uislamu_marekani
Kituo cha Kiislamu katika jimbo la Florida Marekani kimeteketezwa moto na watu wenye chuki dhidi ya Uislamu.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Sep 13, 2016 03:12 UTC
  • Msikiti wateketezwa  moto na wenye chuki dhidi ya Uislamu Marekani

Kituo cha Kiislamu katika jimbo la Florida Marekani kimeteketezwa moto na watu wenye chuki dhidi ya Uislamu.

Kituo cha Kiislamu katika eneo la Fort Pierce, Kaunti ya St Lucie kilitetekea moto Jumatatu wakati Waislamu walikuwa wanajitayarisha kusherehekea Siku Kuu ya Idul Adha.

Moto huo mkali uliharibu paa la ukumbi asili wa msikiti na polisi wanasema wanamtafuta mtu aliyetambuliwa kuwa 'Mzungu mwenye asili ya Kihispania' ambaye ni mshukiwa mkuu wa hujuma hiyo.

Kitendo hicho kimelaaniwa na Waisalmu wa Marekani ambao wamebainisha wasiwasi wao kuhusu kuongezeka vitendo vya chuki dhidi yao.

Mpinzani wa chuki dhidi ya Uislamu

Baraza la Mahusiano ya Kiislamu na Marekani (CAIR) limesema vitendo kama hivyo vimepelekea Waislamu kukabiliwa na wasi wasi mkubwa kwani hawajui ni wapi na ni lini watashambuliwa, Msemaji wa CAIR mjini Florida Wilfredo Amr Ruiz amesema Waislamu wamesikiishwa na hujuma hiyo iliyojiri wakikaribia kusherehekea siku kuu yao kubwa zaidi. Hujuma hiyo ilisadifiana na kumbukumbu ya mwaka wa 15 tokea yajiri mashambulio ya Septemba 11 mwaka 2001 jambo ambalo limepelekea maafisa wa usalama waanzishe uchunguzi kubaini iwapo kuna uhusiano wa matukio hayo mawili.