Wanasiasa wa Marekani ni watumishi wa utawala wa Kizayuni
-
Dk Kevin Barret
Mchambuzi mmoja maarufu wa nchini Marekani amesema kuwa, wanasiasa wa Marekani wapo kwa ajili ya kuutumikia utawala wa Kizayuni wa Israel.
Dk Kevin Barrett alisema hayo jana (Jumapili) wakati alipohojiwa na televisheni ya Press TV na kuongeza kuwa, taasisi zote za kisiasa za Marekani zimekuwa zikitumikia matakwa ya utawala wa Kizayuni kwa miaka na miongo mingi sasa.
Mwandishi, mchambuzi na mtaalamu wa ulimwengu wa Kiislamu amesema kuwa, kwa muda mrefu sasa utawala wa Kizayuni umekuwa ukifanya mauaji dhidi ya Wapalestina kwa kutumia kodi zinazotolewa na wavuja jasho wa nchini Marekani.
Dk Barrett ambaye pia ni mwanachama mwanzilishi wa Muungano wa Waislamu-Wakristo-Mayahudi wa nchini Marekani ameongeza kuwa, huko nyuma mgombea Urais kwa tiketi cha chama cha Republican alisema bila ya kuficha kuwa, kama atachaguliwa kuwa Rais wa Marekani, atahakikisha anakuwa karibu sana na Israel.
Amesema, si jambo la kushangaza kusikia maneno hayo kwani huo ndio uhalisia wa taasisi zote za kisiasa za Marekani tena kwa miaka na miongo mingi sasa.