Kimbunga cha Matthew chaingia kwa kasi Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i17062-kimbunga_cha_matthew_chaingia_kwa_kasi_marekani
Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na kimbuga cha Matthew nchini Marekani imeongezeka na kupindukia watu 13, huku tufani hiyo iliyotokea eneo la Carribean ikiendelea kusababisha maafa makubwa nchini Marekani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 09, 2016 04:50 UTC
  • Kimbunga cha Matthew chaingia kwa kasi Marekani

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na kimbuga cha Matthew nchini Marekani imeongezeka na kupindukia watu 13, huku tufani hiyo iliyotokea eneo la Carribean ikiendelea kusababisha maafa makubwa nchini Marekani.

Habari zinasema kuwa, watu milioni 2.2 wameathirika moja kwa moja na kimbunga hicho kusini mashariki mwa pwani ya Marekani. Majimbo yaliyoathirika zaidi na janga hilo la kimaumbile nchini Marekani ni Carolina, Florida na Georgia.

Athari za kimbunga cha Matthew, Haiti

Hii ni katika hali ambayo, timu za waokoaji zimesema kimbunga hicho kikali zaidi kuwahi kutokea katika muongo mmoja uliopita katika eneo la Carribean kimeshaua watu zaidi ya 900 nchini Haiti, kinyume na takwimu za awali za watu 500.

Maafa ya kimbunga hicho cha Matthew yamesababisha kuakhirishwa uchaguzi wa rais uliokuwa umepangwa kufanyika leo Jumapili katika kisiwa hicho.

Itakumbumwa kuwa, zaidi ya watu laki mbili walifariki dunia mwaka 2010 baada ya mji mkuu wa kisiwa hicho Port-au-Prince kukumbwa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7 kwa kipimo cha rishta.