Marekani hailipi uzito suala la vita dhidi ya ugaidi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i18190-marekani_hailipi_uzito_suala_la_vita_dhidi_ya_ugaidi
Alauddin Burujerdi Mkuu wa Kamati ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, amesema Marekani hailipatii uzito suala la vita dhidi ya ugaidi katika eneo la Mashariki ya Kati.
(last modified 2024-06-10T09:25:34+00:00 )
Oct 26, 2016 08:11 UTC
  • Marekani hailipi uzito suala la vita dhidi ya ugaidi

Alauddin Burujerdi Mkuu wa Kamati ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, amesema Marekani hailipatii uzito suala la vita dhidi ya ugaidi katika eneo la Mashariki ya Kati.

Burujerdi aliyasema hayo Jumanne wakati akihutubu katika Akademia ya Kimataifa ya Udiplomasia huko Paris, Ufaransa na kuongeza kuwa,  Iran ina shaka kuhusu iwapo Marekani iko jadi katika vita dhidi ya ugaidi katika eneo.

Akibainisha zaidi, Burujerdi amesema muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani kwa lengo la kukabiliana na magaidi wa ISIS umekuwa ukilenga Jeshi la Syria.

Mbunge huyo wa ngazi za juu katika Bunge la Iran amesema, katika kipindi cha miaka minane ya vita vya kulazimishwa vya Saddam dhidi ya Iran, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo pia wakati huo ilikuwa chini ya vikwazo, ilipata funzo la ulazima wa kujitegemea katika sekta ya ulinzi sambamba na kuwategemea wananchi.

Rais wa Ufaransa akiwa na Rais wa Iran

Kwingineko katika hotuba yake, Mkuu wa Kamati ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, ameashiria uhusiano wa Tehran na Paris na kusema, safari ya mwezi Januari ya Rais Hassan Rouhani wa Iran nchini Ufaransa ni jambo ambalo lilifungua ukurasa mpya katika uhusiano wa nchi mbili.

Burujerdi aidha amesisitiza kuwa sera za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuwa na uhusiano na nchi za Ulaya na Magharibi kwa ujumla kwa msingi wa kuheshiiana pande mbili.