Trump: Mfumo unaotawala Marekani ni fisadi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i19021-trump_mfumo_unaotawala_marekani_ni_fisadi
Donald Trump mgombea wa kiti cha urais Marekani kwa tikiti ya chama cha Republican ameutaja kuwa fisadi mfumo unaotawala nchini humo.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Nov 08, 2016 01:18 UTC
  • Trump: Mfumo unaotawala Marekani ni fisadi

Donald Trump mgombea wa kiti cha urais Marekani kwa tikiti ya chama cha Republican ameutaja kuwa fisadi mfumo unaotawala nchini humo.

Akizungumza jimboni Florida Jumatatu katika mkutano wa kampeni kabla ya uchaguzi wa rais hii leo, Trump amesema uchaguzi huu utaweka wazi iwapo Marekani itaendelea kutawaliwa na mfumo fisadi au la.

Trump ameongeza kuwa, mgombea wa kiti cha urais wa tikiti ya chama cha Democrat, Hillary Clinton ameiaibisha Marekani na kwamba hakupaswa kupewa idhini ya kugombea urais. Aidha Trump ambaye amekuwa akitabiri kuwa kutakuwa na wizi wa kura katika uchaguzi amekosoa vikali  mahakama za Marekani ambazo amesema zinakejeliwa na walimwengu.

Trump na Clinton

Wakati huo huo, akizungumza katika siku ya mwisho ya kampeni zake Jumatatu katika jimbo la Pennsylvania Hillary Clinton amemtaja Trump kuwa mtu ambaye kiakili hafai kuwa rais na amiri jeshi mkuu.

Uchunguzi wa maoni unaonyesha kutakuwa na mchuano mkali baina ya wagombea hao wawili katika upigaji kura huku Trump akisema mara kadhaa kuwa uchaguzi wa leo utakumbwa na wizi wa kura. Katika mdahalo wake na Clinton mwezi Oktoba, Trump alikataa kuahidi kukubali matokeo ya uchaguzi akishindwa.