Sanders: Mfumo wa ubaguzi ukomeshwe Marekani
Bernie Sanders anayewania nafasi ya kugombea kiti cha rais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Demicratic amesema nchi yake inapaswa kukomesha mfumo usiofaa wa mahakama na ubaguzi unaofanyika kwa mpangilio maalumu.
Bernie Sanders ameashiria hali mbaya ya Wamarekani weusi na kusema idadi kubwa ya Wamarekani weusi ina wasiwasi kuhusu maisha yao ya kila siku.
Sanders amekosoa mwenendo mbaya wa polisi dhidi ya Wamarekani weusi na kusema raia hao wanaandamwa zaidi na polisi kuliko wenzao wazingu.
Bernie Sanders amesema atatoa kipaumbele katika kurekebisha mfumo usiofaa wa mahakama na kupambana na ubaguzi wa aina zote nchini Marekani.
Idadi si ndogo ya Wamarekani weusi huuawa kila mwaka kutokana na ukatili wa polisi wazungu w anchi hiyo.