Russia: Magharibi iache kuingilia Mashariki ya Kati
https://parstoday.ir/sw/news/world-i20542-russia_magharibi_iache_kuingilia_mashariki_ya_kati
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amezitaka nchi za Magharibi ziache kuingilia masuala ya eneo la Mashariki ya Kati.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 01, 2016 07:49 UTC
  • Russia: Magharibi iache kuingilia Mashariki ya Kati

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amezitaka nchi za Magharibi ziache kuingilia masuala ya eneo la Mashariki ya Kati.

Akizungumza katika mahojiano na gazeti la Kiitalia la Coriera de  la Sera, Sergei Lavrov Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa nchi za Magharibi zinapasa kuacha kufanya njama za kubadili muundo wa jiopolitiki wa eneo la Mashariki ya Kati.  

Sergei Lavrov Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia  amezungumzia kadhia ya Syria na kuongeza kuwa, mgogoro wa nchi hiyo utapatiwa ufumbuzi na Wasyria wenyewe na kwamba haki ya kujitawala na umoja wa ardhi ya nchi ya Syria inapasa kuheshimiwa. Katika mahojiano hayo Lavrov amegusia pia uchaguzi wa Rais wa Marekani na kusema,  timu ya siasa za nje ya Rais mteule wa Marekani Donald Trump inapasa kuchukua hatua za kivitendo kuhuisha uhusiano na kuendeleza mapambano dhidi ya ugaidi.