IAEA yathibitisha kuwa Iran imefungamana na JCPOA
(last modified Wed, 07 Dec 2016 07:22:57 GMT )
Dec 07, 2016 07:22 UTC
  • IAEA yathibitisha kuwa Iran imefungamana na JCPOA

Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA umesema hatua ya Iran kuuza nje ya nchi maji mazito ya nyuklia ni katika sehemu ya kuonyesha kufangamana kwake na makubaliano ya nyuklia.

Ripoti ya siri ya IAEA imefichua kuwa, wakala huo ulikagua mpango wa Iran kuiuzia Oman tani 11 za maji mazito ya nyuklia, mauzo yaliyofanyika Novemba 19. Ripoti hiyo ya IAEA imeongeza kuwa, mpango huo wa Iran wa kuuza tani 11 za maji yake mazito kumepelekea akiba ya bidhaa hiyo kuwa chini ya tani 130, jambo ambalo lilianishwa katika makubaliano ya nyuklia yaliyosainiwa huko Vienna nchini Austria Julai mwaka jana, kati ya Iran na nchi za kundi la 5+1.

Kiwanda cha maji mazito ya nyuklia cha Iran

Novemba 22, Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran IAEO, Ali Akbar Salehi alithibitisha kuwa Iran imeuzia Oman tani 11 za maji mazito ya nyuklia.

Ripoti ya mwezi Novemba ya Wakala wa Kimataifa ya Nishati ya Atomiki ilisema kuwa hifadhi ya maji mazito ya Iran imepita kwa kiasi kidogo kiwango kilichoafikiwa katika makubaliano ya nyuklia yajulikanayo kama JCPOA, cha tani 130, na kwamba baada ya kuiuzia Oman tani 11, kiwango cha sasa kinaashiria kuwa Tehran imefungamana na mapatano hayo, yaliyoanza kutekelezwa Januari mwaka huu.

Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran IAEO, Ali Akbar Salehi 

Mbali na Oman, Marekani na Russia zimetangaza utayarifu wao wa kununua maji mazito ya nyuklia kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

 

Tags