Somalia yakosoa marufuku ya kuingia Marekani dhidi ya Waislamu
Rais wa Somalia amekosoa amri mpya iliyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani inayowazuia raia kutoka nchi kadhaa za Kiislamu kuingia Marekani.
Rais Mohamed Abdullahi Farmajo ambaye ana uraia wa nchi mbili za Somalia na Marekani jana wakati wa safari ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo kwamba alikosoa amri hiyo ya Trump na kutoa wito wa kufutwa kabisa.
Mohamed Abdullahi Farmajo ambaye ameishi kwa miaka mingi nchini Marekani amesema Wasomali wamesaidia uchumi na jamii ya nchi hiyo kwa msingi huo idadi ndogo ya wale wanaoweza kusababisha matatizo wanapaswa kushughulikia kivyao.
Akizungumzia changamoto za usalama zinazoikabili nchi hiyo, Rais wa Somalia amesema serikali yake imeelekeza juhudi zake katika namna ya kulishinda kundi la kigaidi la al Shabab.
Amri mpya iliyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani inawazuia raia wa nchi 6 za Kiislamu ikiwemo Somalia, Sudan na Iran kuingia katika ardhi ya Marekani.