Ulaya yaongoza kwa mitandao ya picha za kubakwa watoto
https://parstoday.ir/sw/news/world-i27256-ulaya_yaongoza_kwa_mitandao_ya_picha_za_kubakwa_watoto
Uchunguzi uliofanyika nchini Uingereza umebaini kuwa, bara la Ulaya limechukua nafasi ya nchi za America ya Kaskazini kama kituo kikuu cha kueneza picha na video za kubakwa na kunajisiwa watoto wadogo.
(last modified 2026-06-22T10:26:06+00:00 )
Apr 04, 2017 03:07 UTC
  • Ulaya yaongoza kwa mitandao ya picha za kubakwa watoto

Uchunguzi uliofanyika nchini Uingereza umebaini kuwa, bara la Ulaya limechukua nafasi ya nchi za America ya Kaskazini kama kituo kikuu cha kueneza picha na video za kubakwa na kunajisiwa watoto wadogo.

Uchunguzi huo uliofanywa na Taasisi ya Usimamizi wa Mitandao ya Intaneti unaonesha kuwa, picha na mikanda ya video za kunajisiwa na kubakwa watoto zilizooneshwa mwaka jana wa 2016 barani Ulaya ni asilimia 60 ya matangazo yote ya mtandaoni duniani na kwamba kiwango hicho kimeongezeka kwa asilimia 19 ilikinganishwa na mwaka wa kabla yake. Ripoti ya taasisi hiyo imesema kuwa asilimia 37 ya matangazo ya ntandao wa intaneti yaliyotolewa eneo la America ya Kaskazini mwaka uliopita wa 2016 yalikuwa ya picha za kubakwa na kunajisiwa watoto wadogo. 

Ripoti hiyo pia imesema kiwango cha mauzo ya picha na video za kubakwa na kunajisiwa watoto kimeongezeka kwa asilimia 258 mwaka uliopita ikilinganishwa na mwaka wa kabla yake.

Takwimu hizi za kutisha zinaonesha mporomoko mkubwa na utovu wa maadili unaoendelea kuitafuna jamii ya nchi za Magharibi sambamba na mwelekeo unaoshajiishwa na taasisi za mitazamo ya kisekulari katika nchi hizo wa kupiga vita dini na mafundisho ya Mitume wa Mwenyezi Mungu.