Marekani yakiri kuisadia kijeshi Saudi Arabia katika uvamizi huko Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/world-i27972-marekani_yakiri_kuisadia_kijeshi_saudi_arabia_katika_uvamizi_huko_yemen
Waziri wa Ulinzi wa Marekani amekiri kuwa nchi hiyo inaisaidia kijeshi Saudi Arabia katika vita vyake vya kichokozi dhidi ya Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 19, 2017 02:53 UTC
  • Marekani yakiri kuisadia kijeshi Saudi Arabia katika uvamizi huko Yemen

Waziri wa Ulinzi wa Marekani amekiri kuwa nchi hiyo inaisaidia kijeshi Saudi Arabia katika vita vyake vya kichokozi dhidi ya Yemen.

James Mattis amesema kuwa Marekani licha ya kuwasaidia wanajeshi wa Saudia katika vita huko Yemen, pia inalipa jeshi la Saudia msaada wa kiintelijensia kwa ajili ya kutekeleza mashambulizi mengi ya anga nchini humo. Wakati huo huo James Mattis amekataa kujibu maswali ya waandishi habari waliotaka kufahamu kuhusu uwezekekano wa kuzidishwa misaada ya kijeshi ya Washington kwa Riyadh na kudai kuwa, Marekani inaunga mkono kufanyika mazungumzo ya amani huko Yemen. 

Maafa ya mashambulizi ya Saudia huko Yemen 

Utawala wa Aal Saud ulianzisha hujuma ya kijeshi huko Yemen kwa uungaji mkono wa Marekani na baadhi ya nchi za Kiarabu katika eneo tangu mwezi Machi mwaka juzi lengo likiwa ni kumrejesha madarakani kibaraka wao Rais mstaafu wa Yemen, Abdu Rabbuh Mansour Hadi. Wayemen wanaokaribia 11,000 wameuliwa na wengine wasiopungua milioni tatu wamekuwa wakimbizi kufuatia mashambulizi hayo ya Saudia na waitifaki wake dhidi ya nchi hiyo maskini ya Kiarabu. Miundombinu ya Yemen pia imeharibiwa pakuwa kufautia uvamizi wa kijeshi wa Saudi Arabia. 

Miundombinu ya barabara ilivyoharibiwa na mashambulizi ya anga ya Saudi Arabia huko Yemen