Watu 8 wauawa Marekani katika vitendo vya uhalifu
Watu 8 wameuawa na wengine kujeruhiwa Alhamisi usiku katika vitendo vya uhalifu katika majimbo mbali mbali ya Marekani.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IRIB, mauaji hayo yamejiri katika ufatulianaji risasi katika mji wa Albany jimboni, Georgia, mji wa East Chicago katika jimbo la Indiana na mji wa Smyrna katika jmbo ls Georgia.
Aidha polisi katika mji wa Dardanelle jimboni Arkansas wametangaza kuwa, kufuatia ufatulianaji risasi katika viunga vya mji huo, watu watatu wameuawa.
Kwingineko katika jimbo la Springfield, Massachusetts, mtu moja ameuawa baada ya kufuatulia risasi na watu wasiojulikana huku katika mji wa Sacramento huko California watu wawili wakijeruhiwa baada ya kupigwa risasi. Majimbo mengine ya Marekani pia yameshuhudia vitendo kadhaa vya uhalifu.
Tangu ulipoanza mwaka uliopita wa 2016 hadi sasa, zaidi ya matukio 50,000 ya mashambulio ya ufyatuaji risasi yameripotiwa nchini Marekani ambapo watu karibu 14,000 wameuliwa na wengine zaidi 27,000 wamejeruhiwa.
Hali ya usalama nchini Marekani imezidi kuwa mbaya hasa baada ya kuingia madarakani Rais Donald Trump, biashara ya silaha za moto nchini humo imeongezeka sana kwa namna ambayo haijawahi kushuhudiwa mfano wake.
Kwa mujibu wa ripoti ya Polisi ya Upelelezi Marekani FBI, katika mwezi wa Aprili 2017 pekee, kumeuzwa silaha za moto zaidi ya milioni mbili na 45 elfu, kiwango ambacho kimevunja rekodi ya mauzaji ya silaha nchini humo.