Nchi za Magharibi zinafaidika na biashara ya mihadarati Afghanistan
https://parstoday.ir/sw/news/world-i29682-nchi_za_magharibi_zinafaidika_na_biashara_ya_mihadarati_afghanistan
Mashirika ya kijasusi ya nchi za Magharibi yanafaidika na biashara ya mihadarati nchini Afghanistan, imebainika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 27, 2017 23:14 UTC
  • Nchi za Magharibi zinafaidika na biashara ya mihadarati Afghanistan

Mashirika ya kijasusi ya nchi za Magharibi yanafaidika na biashara ya mihadarati nchini Afghanistan, imebainika.

Kwa mujibu wa Jenerali Masoud Zahedian, Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Mihadarati katika Jeshi la Polisi Iran, tokea Marekani iivamie kijeshi Afghanistan mwka 2001, uzalishaji wa dawa za kulevya au mihadarati aina ya afiuni umeongezeka mara 22. Aidha amesema mwaka 2001 uzalishaji afiuni Afghansitan ulikuwa karibu tani 200 kwa mwaka lakini leo, pamoja na kuwepo wanajeshi wa Marekani na wale wa muungano wa kijeshi wa NATO nchini Afghanistan, nchi hiyo inazalisha tani 4,400 za afiuni kwa mwaka na inatabiriwa kiwango hicho kitafikia tani 7,700 mwaka huu wa 2017.

Brigedia Zahedian amesema Iran inaongoza duniani katika vita dhidi ya mihadarati. Amesema Iran imeweka viziuzi kadhaa katika mipaka yake  ili kuzuia wabeba mihadarati kupita. Aidha amesema hadi sasa maafisa usalama Wairani wapatao 3,800 wameuawa shahidi na wengine 12,000 kujeruhiwa katika mapabano na wasafirishaji wa dawa za kulevya.

Wanajeshi wa Marekani wakiwa katika shamba la mihadarati aina ya afiuni nchini Afghanistan

Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Mihadarati katika Jeshi la Polisi ya Iran ameashiria kuzembea nchi za Magharibi katika kutekekeleza majukumu yao ya kimataifa ya kupambana ipasavyo na dawa za kulevya na kusema: "Pamoja na kuwepo jitihada zisizo na kikomo za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, nchi za Ulaya zinaonyesha kutojali katika vita dhidi ya mihadarati."

Taasisi za kimataifa zinazofungamana na Umoja wa Mataifa zimekiri kuwa Iran inaongoza katika via dhidi ya mihadarati duniani.