Seneti ya Marekani yaakhirisha kura kuhusu vikwazo vipya dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i30232-seneti_ya_marekani_yaakhirisha_kura_kuhusu_vikwazo_vipya_dhidi_ya_iran
Seneti ya Marekani imeakhirisha kuupigia kura mpango wa vikwazo vipya vya upande mmoja dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hadi Jumatatu tarehe 12 mwezi huu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 09, 2017 03:32 UTC
  • Seneti ya Marekani yaakhirisha kura kuhusu vikwazo vipya dhidi ya Iran

Seneti ya Marekani imeakhirisha kuupigia kura mpango wa vikwazo vipya vya upande mmoja dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hadi Jumatatu tarehe 12 mwezi huu.

Katika kikao chao cha Jumatano iliyopita, wawakilishi 91 wa Seneti ya Marekani walipasisha suala la kujadili mpango wa vikwazo vipya vya upande mmoja dhidi ya Iran. Baada ya upigaji kura, kulikuwa na muda wa masaa 30 ya kuendeleza mazungumzo katika uwanja huo, hata hivyo suala hilo halikuwekwa kwenye ajenda ya Seneti siku ya Alhamisi na hivyo mpango huo umeakhirishwa kupigiwa kura ya mwisho hadi Jumatatu ijayo. 

Seneti ya Marekani kupiga kura ya mwisho kuhusu mpango wa vikwazo vya upande mmoja dhid ya Iran 

Japokuwa wale wanaounga mkono suala la Iran kuwekewa vikwazo vipya kwa kisingizio cha kukiuka haki za binadamu na kuhusika na vitendo vya kigaidi wanadai kuwa, mpango huo hauathiri utekelezaji wa makubaliano ya nyuklia, lakini baadhi ya wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, hatua hiyo itaandaa uwanja wa kukiukwa makubaliano ya JCPOA na wanatahadharisha kuhusu taathira zitakazojitokeza baada ya kuidhinishwa mpango wa vikwazo vipya dhidi ya Iran.

Iwapo mpango huo utaidhinishwa, wawakilishi wa Bunge la Marekani watapasa kuupasisha na kusainiwa na Rais. 

Makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yanailazimisha Marekani kutupilia mbali utekelezaji na kujiepusha kuweka vikwazo vilivyoondolewa na makubaliano hayo.