UEI: Ikiwa Trump atashinda basi uchumi wa dunia utakuwa mashakani
Asasi ya Intelejensia ya Uchumi 'Unit Economist Intelligence' inayojihusisha na utafiti wa masuala ya uchumi, imetahadharisha kuwa, ikiwa Donald Trump atashinda katika uchaguzi ujao wa rais nchini Marekani, basi uchumi wa dunia utakuwa mashakani.
Asasi hiyo ya kiintelejensia katika masuala ya uchumi duniani imesema hayo katika ripoti yake ya jana na kuongeza kuwa, uchunguzi uliofanywa unaonyesha kuwa, iwapo Trump anayewania kuteuliwa na chama chake cha Republican kugombea urais nchini Marekani atashindwa, basi suala hilo litahatarisha sana uchumi wa dunia. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ushindi wa mwanasiasa huyo, utasababisha pia mgogoro mkubwa wa kisiasa na kiusalama nchini Marekani na ulimwengu kwa ujumla. Utabiri uliofanywa na taasisi hiyo unaonyesha kuwa, utawala wa Trump ambao utakuwa wa vita, utaathiri pakubwa biashara, kukatika mahusiano ya kibiashara kati ya Marekani na mataifa mengine ya dunia, na kuongezeka maradufu makundi ya kigaidi duniani. Ripoti hiyo imekutaja kuporomoka uchumi wa China, matatizo ya uchumi katika eneo la ukanda wa EURO na uwezekano wa Uingereza kujitoka katika Umoja wa Ulaya ni mambo matatu makuu yanayotishia uchumi wa dunia hivi sasa.