Aug 20, 2017 06:50 UTC
  • Russia: Marekani na NATO zinaruhusu magendo ya dawa za kulevya Afghanistan

Serikali ya Russia imetangaza kuwa, hatua ya Marekani na jumuiya ya kijeshi ya nchi za Magharibi NATO ya kutopambana na dawa za kulevya nchini Afghanistan licha ya kushadidi uzalishaji na magendo ya dawa hizo, inatia shaka na kustaajabisha.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imeeleza kusikitishwa na ongezeko linalotia wasiwasi la uzalishaji na magendo ya dawa za kulevya nchini Afghanistan na kusema kuwa: Ni jambo linalotia shaka na kushangaza kuona askari wa Marekani na jeshi la NATO lililoko Afghanistan halipambani na magendo ya dawa za kulevya nchini humo.

Kwa kutegemea takwimu zilizotolewa na Umoja wa Mataifa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesema kuwa: Karibu nusu ya pato la makundi haramu nchini Afghanistan ambalo linafikia dola milioni 400 linatokana na magendo ya dawa za kulevya. dawa

Magendo ya dawa za kulevya imeongezeka Afghanistan licha ya kuwepo maelfu ya askari wa Marekani nchini humo

Taarifa hiyo imeitaka Marekani kupanga stratijia maalumu ya kupambana na dawa za kulevya nchini Afghanistan. 

Marekani iliishambulia Afghanistan mwaka 2001 kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na kurejesha amani nchini humo. Hata hivyo tangu wakati huo machafuko, ugaidi, uzalishaji na magendo ya dawa za kulevya vimeongezeka kwa kiwango kikubwa nchini Afghanistan.  

Tags