Mahakama ya Pakistan: Musharaf anasakwa katika kesi ya mauaji ya Bhutto
https://parstoday.ir/sw/news/world-i33849-mahakama_ya_pakistan_musharaf_anasakwa_katika_kesi_ya_mauaji_ya_bhutto
Rais wa zamani wa Pakistan, Parvez Musharaf anasakwa na vyombo vya sheria vya nchi hiyo kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwaka 2007 ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Pakistan Bi Benazir Bhutto.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 01, 2017 03:45 UTC
  • Mahakama ya Pakistan: Musharaf anasakwa katika kesi ya mauaji ya Bhutto

Rais wa zamani wa Pakistan, Parvez Musharaf anasakwa na vyombo vya sheria vya nchi hiyo kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwaka 2007 ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Pakistan Bi Benazir Bhutto.

Mahakama ya kupambana na ugaidi katika mji wa Rawalpindi jana ilitoa dekree hiyo ikiwa imepita miaka minne baada ya jenerali huyo wa zamani kutajwa katika tuhuma za mauaji ya Benazir Bhutto. 

Kesi hiyo ilichelewa kutokana na matatizo ya kiafya ya Musharaf. Rais huyo wa zamani wa Pakistan aliondoka nchini humo mwaka 2016 na kuelekea nje ya nchi kwa ajili ya matibabu, na amekuwa akiishi Dubai Imarati.

Parvez Musharaf ambaye alikuwa kiongozi mkuu wa nchi wakati Bi Bhutto alipouawa, amekuwa akishukiwa kwa muda mrefu kuhusika katika mauaji hayo yaliyohusisha mlipuko wa bomu na ufyatuaji risasi uliosababisha kifo cha Benazir Bhutto, Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan pamoja na makumi ya raia waliokuwa wamehudhuria mkutano wake wa kampeni za uchaguzi.

Mwendazake bi Benazir Bhutto Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan

Mahakama hiyo ya kupambana na ugaidi huko Rawalpindi pia imewahukumu maafisa polisi kadhaa wa zamani kifungo cha miaka 17 jela na kuwatoza faini ya dola 5000 huku ikiwafutia mashtaka washukiwa wengine watano wenye misimamo mikali.  Uamuzi huo umepingwa vikali na Aseefa B. Zardari binti wa mwendazake Benazir Bhutto.