Russia yaapa kujibu vikali uadui wa Marekani
Waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergei Lavrov amesema kuwa, nchi hiyo itajibu vikali hatua za kiuadui za Marekani zinazoilenga Russia.
Lavrov alikuwa akizungumzia hatua ya Marekani ya kufunga ubalozi mdogo wa Russia huko San Fransisco, na ofisi nyingine mbili za ziada za kibalozi mjini Washington na New York ifikapo kesho. Hatua hiyo ya Marekani imetokana na uamuzi wa Russia wa kupunguza wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani nchini humo kuendana na idadi ya wanadiplomasia wa Russia nchini Marekani. Hata hivyo, Lavrov hakufafanua hatua itakayochukuliwa na Russia.
Hivi karibuni Rais Vladimir Putin wa Russia aliagiza wanadiplomasia 755 wa Marekani kuondoka Russia baada ya bunge la Marekani kuweka vikwazo vipya dhidi ya Russia kwa tuhuma za kuingilia uchaguzi wa nchi hiyo mwaka jana.
Russia ilichukua hatua hizo kujibu vikwazo vipya vya Marekani dhidi yake na pia serikali ya Moscow imetoa amri ya kupunguzwa idadi ya wanadiplomasia wa Marekani nchini humo sambamba na kuzuia baadhi ya mali za kidiplomasia za maafisa hao.