Uchunguzi: Vijana wa Kiislamu nchini Uingereza wanabaguliwa katika kila sekta
(last modified Thu, 07 Sep 2017 14:25:30 GMT )
Sep 07, 2017 14:25 UTC
  • Uchunguzi: Vijana wa Kiislamu nchini Uingereza wanabaguliwa katika kila sekta

Uchunguzi mpya wa hivi karibuni unaonyesha kwamba, vijana wa Kiislamu wanaoishi nchini Uingereza wamekuwa wahanga wakubwa wa vitendo vya ubaguzi kuanzia shuleni, vyuo vikuu na hata maeneo ya kazi.

Kamisheni ya Harakati ya Kijamii nchini Uingereza Alkhamis ya leo imetoa ripoti ya uchunguzi uliofanywa na Chuo Kikuu cha Sheffield ambapo imeonya kwamba ni asilimia ndogo sana ya vijna wa Kiislamu ambao wanaweza kupata kazi ndani ya taifa hilo wakilinganishwa na vijana wenzao wa imani nyingine za kidini. Imefafanua kuwa, vijana hao wamekuwa wakinyimwa fursa za kuonyesha uwezo wao katika soko la kazi.

Baadhi ya viongozi wa kisiasa wakijifanya kuwatoa wasi wasi vijana wa Kiislamu

Uchunguzi huo uliofanywa na Chuo Kikuu cha Sheffield umesisitiza kuwa, chuki dhidi ya Uislamu na ubaguzi wa kidini unaoshuhudiwa hii leo katika jamii ya Uingereza, ni kikwazo kikuu katika njia ya vijana Waislamu kufikia malengo yao. Aidha matokeo ya uchunguzi huo yanaonyesha kwamba, vijana wa Kiislamu ni wenye kufanya kazi kwa bidii, wapole na wenye matarajio ya kufikia malengo, huku akthari yao wakiwa wanaamini kuwa, kutokana na ubaguzi wa kidini uliokithiri, wanalazimika kufanya kazi mara 10 zaidi kuliko wenzao wasiokuwa Waislamu.

Waislamu nchini Uingereza

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa Mwislamu mmoja kati ya watanao nchini Uingereza na eneo la Wales, hufanya kazi kwa muda mrefu huku asilimia sita tu kati yao wakiwa ndio wanaofanikiwa kufikia daraja za juu za uongozi nchini humo. Kwa sasa Waislamu milioni tatu wanaishi nchini Uingereza.

Tags