WFP: Hakuna usawa katika ugawaji chakula duniani, umasikini unatia wasi wasi
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula la WPF limetoa ripoti likielezea kutokuwepo usawa katika ugawaji chakula na kwamba ongezeko la umasikini katika maeneo tofauti ya dunia ni lenye kutia wasi wasi mkubwa.
Taarifa hiyo ya WFP ambayo imejikita katika kuelezea uhalisia wa hali mbaya ya gharama za chakula duniani, imetoa mfano kwa kusema kuwa, ahadi ya chakula iliyotolewa kwa ajili ya masikini mmoja wa mji wa New York Marekani ilikuwa ni kiasi cha Dola 1.2 katika hali ambayo masikini wa Sudan Kusini ni Dola 321.
Kufuatia hali hiyo, David Bessley mkuu wa utekelezaji wa WFP amesema kuwa, baada ya wataalamu wa shirika hilo kulinganisha ukubwa wa manunuzi ya chakula katika nchi tofauti, wamegundua kutokuwepo usawa kwa kiasi kikubwa miongoni mwa nchi kadhaa kuhusiana na ahadi za mgao wa chakula. Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa WPF zinaonyesha kwamba chanzo cha idadi kubwa ya watu wanaoteseka kwa njaa duniani, ni vita, ukosefu wa uthabiti wa kisiasa, udhaifu wa miundombinu na mabadiliko ya tabianchi.