Askari wa gadi ya pwani nchini Italia waokoa wahajiri 700
(last modified Sat, 04 Nov 2017 07:48:23 GMT )
Nov 04, 2017 07:48 UTC
  • Askari wa gadi ya pwani nchini Italia waokoa wahajiri 700

Askari wa gadi ya pwani nchini Italia wametangaza kwamba Ijumaa ya jana waliwaokoa wahajiri 700 katika bahari ya Mediterranea.

Maafisa wanoongoza operesheni katika maji ya bahari ndani ya mataifa ya Ulaya wametangaza kuwa Ijumaa ya jana meli moja ya Uhispania iliopoa miili 23 ya wahajiri kutoka majini sambamba na kuwaokoa wengine 64 baada ya chombo walichokuwa wakikitumia kusafiria baharini kuzama. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, operesheni zilitekelezwa katikati ya maji ya bahari ya Mediterranea na karibu na mpaka wa Libya na kusini mwa Ulaya ambapo jumla ya wahajiri 764 waliokolewa. Wahajiri waliookolewa wanatoka nchi za Pakistan, Libya, Bangladesh, Algeria, Misri, Nepal, Morocco, Sri Lanka, Yemen, Syria, Jordan na Lebanon.

Wahajiri wanaohatarisha maisha yao baharini

Hii ni katika hali ambayo Jumatano iliyopita wahajiri wengine 900 waliokolewa na askari hao wa gadi ya pwani mwa Italia. Pwani ya magharibi mwa Libya ni eneo kuu la mwanzo wa harakati za wahajiri haramu kuelea Ulaya ambako wanaamini kwamba wanaweza kupata maisha bora. Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, zaidi ya wahajiri haramu wapatao elfu 18 na 800 wametiwa mbaroni kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu 2017 hadi kufikia tarehe 24 Oktoba katika maji ya Mediterranea. Aidha ripoti hiyo inasema kuwa, zaidi ya wahajiri elfu 11 waliweza kuingia Italia.

Tags