Nov 23, 2017 07:08 UTC
  • Bruno Rodríguez, Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba
    Bruno Rodríguez, Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba

Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba amelaani vitisho na misimamo ya chuki na ya kuzusha fujo vinavyofanywa na Marekani dhidi ya Korea Kaskazini.

Bruno Rodríguez ametoa matamshi hayo katika mazungumzo yake na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini, Ri Yong-ho na kutangaza rasmi msimamo wa Cuba wa kupinga misimamo ya chuki na ya kichokozi ya Marekani dhidi ya Pyongyang.

Rodríguez amesisitiza kuwa, utatuzi wa mgogoro wa Rasi ya Korea utapatikana kwa njia ya mazungumzo na si kwa vitisho vya kijeshi.

Ri Yohg-ho, Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini

 

Kwa upande wake, Ri Yohg-ho, waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini ameelezea kusikitishwa kwake na jinsi Marekani inavyochochea hali ya usalama katika Rasi ya Korea na kusisitiza kuwa, mgogoro wote wa eneo hilo unasabisibishwa na kuweko vikosi vya kijeshi vya Marekani katika ukanda huo.

Mgogoro wa Korea Kaskazini umepamba moto katika miezi ya hivi karibuni kutokana na Marekani kumimina wanajeshi wake katika Rasi ya Korea na kufanya mazoezi ya mara kwa mara ya kijeshi katika eneo hilo kwa kushirikiana na waitifaki wake kama Japan na Korea Kusini.

Marekani na waitifaki wake wanafanyia majaribio silaha zao za kila namna katika Rasi ya Korea na wakati huo huo wanalaani vikali kila pale Korea Kaskazini inapofanyia majaribio silaha zake. Pyongyang inasema haiwezi kuachana na silaha zake za nyuklia na makombora yake maadamu Marekani inaendelea kufanya chokochoko na uadui dhidi ya Korea Kaskazini.

Tags