Kifurushi cha misaada mipya ya Kamisheni ya Ulaya kwa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/world-i39785-kifurushi_cha_misaada_mipya_ya_kamisheni_ya_ulaya_kwa_palestina
Kamisheni ya Ulaya imetangaza wazi misaada yake mipya kwa Palestina inayojumuisha misaada kwa ajili ya kulinda nafasi ya Quds na kuwaunga mkono wananchi wa Palestina kuelekea kuasisi nchi huru ya Palestina kama sehemu ya njia ya kupatikana nchi mbili katika mzozo wa Mashariki ya Kati.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 01, 2018 11:19 UTC
  • Kifurushi  cha misaada mipya ya Kamisheni ya Ulaya kwa Palestina

Kamisheni ya Ulaya imetangaza wazi misaada yake mipya kwa Palestina inayojumuisha misaada kwa ajili ya kulinda nafasi ya Quds na kuwaunga mkono wananchi wa Palestina kuelekea kuasisi nchi huru ya Palestina kama sehemu ya njia ya kupatikana nchi mbili katika mzozo wa Mashariki ya Kati.

Kamisheni ya Ulaya imetoa taarifa na kusistiza kufungamana kwake na Umoja wa Ulaya katika suala la kuunga mkono juhudi za uhuishaji wa kijamii na kiuchumi wa Quds na kueleza kuwa Umoja huo itadhamini kifedha miradi mbalimbali ya kuwawezesha raia wa Palestina katika mji huo kupitia miradi iliyokusudiwa kwa maslahi ya vijana na sekta binafsi. 

Johannes Hahn  Kamishna wa Sera na Masuala ya Ujirani wa Umoja wa Ulaya ameeleza kuwa umoja huo itaendelea kuwaunga mkono Wapalestina katika suala la kuasisi nchi ya Palestina mji mkuu wake ukiwa ni Quds sambamba na kuidhinisha msaada huo mpya wa yuro milioni 42.5. 

Johannes Hahn, Kamishna wa Sera na Masuala ya Ujirani wa EU  
 
Naye Bi Federica Mogherini Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya alisema jana katika kikao huko Brussels  cha nchi wafadhili wa Palestina kuwa hali ya raia wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza inaashiria udharura wa kutolewa misaada ya kibinadamu.