Ujerumani yasisitizia umuhimu wa kufanya mazungumzo na Russia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i42504-ujerumani_yasisitizia_umuhimu_wa_kufanya_mazungumzo_na_russia
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa kufanya mazungumzo na Russia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 01, 2018 12:44 UTC
  • Ujerumani yasisitizia umuhimu wa kufanya mazungumzo na Russia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa kufanya mazungumzo na Russia.

Heiko Maas amesema  hii leo sambamba na kuongezeka mivutano kati ya nchi za Magharibi na Moscow baada ya kufukuzwa wanadiplomasia kulikosababishwa na kitendo cha kupewa sumu Sergei Skripal jasusi wa zamani wa Russia kwamba, milango ya mazungumzo na Russia ingali wazi. 

 Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amedai kuwa, mienendo ya Russia katika miaka ya karibuni imeondoa hali ya kuaminiana. Heiko Maas amesema kuwa wao wapo tayari kufanya mazungumzo na kwamba inawezakana kujenga hali ya kuaminiania hatua kwa hatua iwapo Russia itakuwa tayari.

Siku kadhaa zilizopita Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani alitangaza kuwa, nchi yake inakaribisha mazungumzo na Russia.

Madai ya kupewa sumu Sergei Skripal jasusi wa zamani wa Russia pamoja na binti yake Yulia nchini Uingereza yamesababisha hali ya mvutano katika uhusiano wa Moscow na nchi za Magharibi.

Sergei Skripal akiwa na binti yake, Yulia 

Hivi karibuni Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi ziliwafukuza wanadiplomasia wa Russia katika nchi hizo na kisha Russia pia ikajibu hatua hiyo kwa kuwafukuza wanadiplomasia wa nchi hizo mjini Moscow.