Nchi za Magharibi zakwamisha uchunguzi wa kadhia ya Skripal
https://parstoday.ir/sw/news/world-i42710-nchi_za_magharibi_zakwamisha_uchunguzi_wa_kadhia_ya_skripal
Mwakilishi wa Rusia katika Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali (OPCW) amesema kuwa pendekezo la pamoja la nchi za Russia, Iran na China la kuanzisha uchunguzi mpya kuhusu kadhai ya Sergei Skkripal katika shirika hilo limekataliwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 06, 2018 02:59 UTC
  • Nchi za Magharibi zakwamisha uchunguzi wa kadhia ya Skripal

Mwakilishi wa Rusia katika Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali (OPCW) amesema kuwa pendekezo la pamoja la nchi za Russia, Iran na China la kuanzisha uchunguzi mpya kuhusu kadhai ya Sergei Skkripal katika shirika hilo limekataliwa.

Alexander Shulgin amesema kuwa pendekezo lililotolewa na Russia, China na Iran linaoana kikamilifu na sheria za kimataifa na kuongeza kuwa, Marekani, Uingereza na washirika wao wamezuia kupasishwa pendekezo hilo katika Baraza la Utendaji wa Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali.

Nchi 23 kati ya 41 wanachama wa baraza hilo zimeafiki pendekezo hilo lakini ili kuweza kupasishwa kunahitaji kura za thuluthi mbili ya wajumbe wote 41. Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikkali (OPCW) liliitisha kikao Jumatano iliyopita kwa shabaha ya kuchunguza madai ya Uingereza kwamba Russia ilihusika la jaribio la kutaka kumuua jasusi wa zamani wa nchi hiyo, Sergei Skripal akiwa nchini Uingereza. Tarehe 4 Machi Skripal na binti yake, Yulia wanadaiwa kupewa kile London inachosema ilikuwa sumu ya kemikali katika eneo la Salisbury lililoko kusini magharibi mwa mji mkuu wa Uingereza. London inadai kuwa Russia ndiyo iliyohusika na hujuma hiyo lakini Moscow inakanusha vikali madai hayo na imetangaza kuwa iko tayari kushirikiana na Uingereza kwa ajili ya kubaini uhakika na ukweli. Hata hivyo Uingereza imekataa kutoa ushahidi wa madai hayo na kushirikiana na Russia katika kadhia hiyo.

Skripal na binti yakke, Yulia

Hapa linajitokeza swali kwamba, ni kwa nini nchi za Magharibi zinakwamisha juhudi za kufanyika uchunguzi makini na wa kitaalamu kuhusu madai ya kupewa sumu Sergei Skripal?

Jibu la swali hili ni kwamba, kwa nchi za Magharibi ambazo katika miaka ya hivi karibuni zimekuwa zikifanya mikakati ya kuzidisha mashinikizo na vikwazo dhidi ya Russia, kadhia hiyo ya Skripal imekuwa kisingizio kizuri zaidi kwa ajili ya kukabiliana na Moscow. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, kwa mtazamo wa nchi hizo Russia inaweza kupata pigo na kuchanganyikiwa kutokana na kadhia hiyo.

Hata hivyo tofauti na walivyodhania, Moscow imekwenda mbele zaidi ikitaka kuwekwa wazi uhakika na kweli kuhusu madai ya kupewa sumu ya kemikali Sergei Skripal na sasa mpira uko katika uwanja wa nchi za Magharibi zinazokwepa kutoa ushahidi na hata kukwamisha uchunguzi wa kitaalamu kuhusu madai hayo. Hii ni pamoja na kuwa, wataalamu wa silaha za kemikali wa Uingereza wameshindwa kuthibitisha kwamba, gesi ya neva inayodaiwa kutumiwa dhidi ya Skripal na binti yake ilitengenezwa Russia. Gary Aitkenhead ambaye ni Mkugenzi wa Maabara ya Porton Down ya jeshi la Uingereza amesema kuwa: Uchunguzi uliofanywa na wataalamu wa maabara hiyo haujathibitisha kwamba gesi ya sumu iliyotumiwa dhidi ya Sergei Skripal ilitengenezwa nchini Russia.

Katika upande mwingine imeeleweka kwamba, gesi hiyo ya neva iliyotumiwa dhidi ya Skripal inaweza kuzalishwa katika nchi 20. Katika uwanja huu Rais Vladimir Putin wa Russia anasema: Kwa mujibu wa mtazamo wa wataalamu wa kimataifa, karibu nchi 20 duniani zinaweza kuzalisha gesi ya neva inayoshabihiana na hiyo.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May na Rais Putin wa Russia

Kwa msingi huo si rahisi kuweza kuthibitisha tuhuma kwamba Russia ndiyo iliyotengeneza gesi iliyotumiwa dhidi ya sumu Sergei Skripal.

Ni kutokana na hayo yote na kutokuwa na ushahidi madhubuti wa kuhusika Russia katika kadhia ya kumpa sumu Sergei Skripal ndiyo maana Uingereza, Marekani na washirika wao wakazuia na kukwamisha pendekezo la kuanzishwa uchunguzi mpya kuhusu kadhia hiyo katika Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali.