Mogherini ajibu mchezo wa kitoto wa Netanyahu kuhusu mapatano ya JCPOA
https://parstoday.ir/sw/news/world-i43878-mogherini_ajibu_mchezo_wa_kitoto_wa_netanyahu_kuhusu_mapatano_ya_jcpoa
Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, usiku wa kuamkia leo amejibu mchezo wa kitoto wa Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel aliyedai kuwa eti Iran haijaheshimu mapatano ya nyuklia ya JCPOA.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
May 01, 2018 00:06 UTC
  • Mogherini ajibu mchezo wa kitoto wa Netanyahu kuhusu mapatano ya JCPOA

Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, usiku wa kuamkia leo amejibu mchezo wa kitoto wa Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel aliyedai kuwa eti Iran haijaheshimu mapatano ya nyuklia ya JCPOA.

Akizungumza na waandishi wa habari, Federica Mogherini amesema kuwa, hadi hivi sasa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA umeshatoa ripoti 10 na zote zimesisitiza kuwa Iran imeheshimu kikamilifu mapatano ya nyuklia ya JCPOA wakati ambapo Netanyahu anatoa madai ambayo hayana ushahidi wowote kuhusu kutoshikamana Tehran na mapatano hayo.

Benjamin Netanyahu ni maarufu kwa michezo ya kitoto, hapa anashindwa kuonesha ulipo hasa utawala wa Kizayuni huku akimfanya kucheka hata aliyeko pembeni mwake

 

Mkuu huyo wa siasa za kigeni wa Umoja wa Ulaya pia amesema, wakala wa IAEA ndiyo marejeo pekee kuhusu miradi ya nyuklia ya Iran na wakati wakala huo umethibitisha mara kumi kuwa Iran imeheshimu mapatano hayo, vipi anajitokeza mtu na kudai kinyume chake tena bila ya ushahidi wowote?

Jana usiku, waziri mkuu wa utawala pandikizi wa Kizayuni wa Israel alionesha picha, CD na karatasi akidai kuwa eti Iran inaendesha kwa siri mpango wa kumiliki silaha za nyuklia.

Madai hayo ya uongo ya Netanyahu yametolewa mara baada ya ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo huko Tel Aviv, kama njia ya kuhalalisha nia ya rais wa Marekani ya kujitoa kwenye mapatano hayo.