Mogherini: Kuyadumisha makubaliano ya JCPOA ni mtihani kwa Umoja wa Ulaya
https://parstoday.ir/sw/news/world-i44938-mogherini_kuyadumisha_makubaliano_ya_jcpoa_ni_mtihani_kwa_umoja_wa_ulaya
Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema kuyalinda na kuyadumisha makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) ni mtihani kwa Umoja wa Ulaya.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
May 24, 2018 22:49 UTC
  • Mogherini: Kuyadumisha makubaliano ya JCPOA ni mtihani kwa Umoja wa Ulaya

Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema kuyalinda na kuyadumisha makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) ni mtihani kwa Umoja wa Ulaya.

Federica Mogherini ameyasema hayo katika kikao kilichofanyika kwa anuani ya "Kikao cha Uandaaji Ajira cha Ulaya", ambapo mbali na kuashiria ulazima wa kuyaendeleza makubaliano ya JCPOA amesema, huo ni mtihani kwa Umoja wa Ulaya wa kuweza kuchukua maamuzi yenyewe juu ya mambo yanayoihusu.

Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya ameongeza kuwa: "Inapasa tuonyeshe haki yetu ya mamlaka ya kujitawala, tulinde maslahi yetu na kuonyesha nguvu na uwezo wetu".

Kwa mujibu wa Mogherini, kama walivyo Wairani ambao wameyaheshimu makubaliano ya JCPOA, EU pia inapaswa kuyatekeleza na kuyalinda makubaliano hayo.

Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya ametoa matamshi hayo katika hali ambayo, baada ya Marekani kujitoa kwenye makubaliano ya JCPOA viongozi wa nchi hiyo wamekuwa wakizionya nchi za Ulaya juu ya hatari ya kukabiliwa na vikwazo vya Washington endapo zitashirikiana kiuchumi na Iran.../