Russia yaigaragaza Saudia katika ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i45864-russia_yaigaragaza_saudia_katika_ufunguzi_wa_michuano_ya_kombe_la_dunia
Timu ya taifa ya soka ya Russia imeanza mashindano ya soka ya Kombe la Dunia kwa kishindo baada ya kuigaragaza Saudi Arabia mabao matano kwa nunge katika ufunguzi wa duru ya 21 ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu.
(last modified 2025-11-07T02:31:33+00:00 )
Jun 15, 2018 04:44 UTC
  • Russia yaigaragaza Saudia katika ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia

Timu ya taifa ya soka ya Russia imeanza mashindano ya soka ya Kombe la Dunia kwa kishindo baada ya kuigaragaza Saudi Arabia mabao matano kwa nunge katika ufunguzi wa duru ya 21 ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu.

Katika mchezo huo uliochezwa jana katika kundi la A la michuano hiyo kwenye uwanja wa Luzhniki, mjini Moscow, timu ya Russia ilionyesha mchezo mzuri na wa kusisimua mbele ya watazamani kwa kuifunga Saudia mabao matano bila jibu. Katika kundi A Ijumaa ya leo zitacheza timu za Misri na Uruguay.

Timu ya taifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo nayo ni moja ya timu 32 zinazoshiriki katika michuano katika kundi B inashuka dimbani leo kuchuana na Morocco. Kundi hilo linazishirikisha pia nchi za Uhispania na Ureno .Mechi ya Iran na Morocco inafanyika katika uwanja wa Saint Petersburg nchini Russia.

Saudia na Russia

Katika ufunguzi wa michuano ya kombe la dunia mwaka huu Rais Vladmir Putin wa Russia alisema kuwa zaidi ya watu bilioni moja duniani ni mashabiki wa mpira wa miguu na kwamba watu hao wanafuatilia michuano hiyo.

Zaidi ya vongozi wa nchi 20 walihudhuria sherehe za ufunguzi wa michuano hiyo Alkhamisi ya jana. Miji iliyoandaliwa michuano hiyo ya kombe la dunia mwaka 2018 ni pamoja na Moscow, Saint Petersburg, Kaliningrad, Nizhny Novgorod, Kazan, Samara, Saransk, Volgograd, Rostov, Sochi na Yekaterinburg.