Indonesia: Hakuna mazungumzo ya siri tuliyoyafanya na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/world-i46454-indonesia_hakuna_mazungumzo_ya_siri_tuliyoyafanya_na_israel
Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia imekadhibisha madai yaliyotolewa na utawala haramu wa Kizayuni kwamba serikali ya nchi hiyo imefanya mazungumzo ya siri na utawala huo kwa ajili ya kuondolewa marufuku inayowazuia Wazayuni kufanya safari nchini Indonesia.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 30, 2018 04:16 UTC
  • Indonesia: Hakuna mazungumzo ya siri tuliyoyafanya na Israel

Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia imekadhibisha madai yaliyotolewa na utawala haramu wa Kizayuni kwamba serikali ya nchi hiyo imefanya mazungumzo ya siri na utawala huo kwa ajili ya kuondolewa marufuku inayowazuia Wazayuni kufanya safari nchini Indonesia.

Arrmanatha Nasir, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia ameyasema hayo katika kujibu matamshi ya viongozi wa Kizayuni juu ya kuondolewa marufuku inayozuia kuwapatia vibali vya kuingia Indonesia raia wa utawala haramu wa Israel. Amesisitiza kwamba Indonesia haina uhusiano wowote wa kisiasa na utawala wa Kizayuni kama ambavyo hakuna mazungumzo yoyote ya siri yaliyofanyika kati ya Tel Aviv na Jakarta kwa ajili ya kuondolewa marufuku hiyo.

Arrmanatha Nasir, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia

Kwa mujibu wa uamuzi wa serikali ya Indonesia, marufuku ya kuzuia kuwapatia Wazayuni vibali kwa ajili ya kuingia nchi hiyo, ilianza tarehe 26 Juni mwaka huu. Uamuzi huo ulichukuliwa na Jakarta ikiwa ni kujibu hatua za ukandamizaji uliopindukia wa utawala wa Kizayuni dhidi ya raia madhlumu wa Palestina na kupanuka vitendo vya utumiaji mabavu vya Israel katika eneo la Mashariki ya Kati.